YANGA WAWATULIZA JKT TANZANIA

MCHORA ramani wa Yanga, Kocha Mkuu Miguel Gamondi amekiongoza kikosi hicho kusepa na pointi tatu za wajeda JKT Tanzania kwa ushindi wa mabao 2-0.

Mabao yamefungwa na Pacome dakika ya 23 na Clatous Chama dakika ya 43 kwa pigo la faulo akitumia mguu wa kulia akiwa nje ya 18.

Katika mchezo huo JKT Tanzania nyota wao Dennis Richard ambaye ni kipa alionyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja dakika ya 42 kwa kudaka mpira eneo la nje ya 18.

Ni Gonzo kipa namba mbili aliingia naye alifungwa bao moja tu kipindi cha kwanza na kipindi cha pili timu zote zilikuwa imara huku ukichezwa mpira mkubwa kwa kila timu.

Shukran kwa Djigui Diarra kwa kuwa kikwazo kwa washambuliaji wa JKT Tanzania na kitendo cha kuonekana akipoteza muda dakika ya 89 kilimfanya mwamuzi Arajiga akamuonyesha kadi ya njano.

Pointi 18 kwa Yanga ambao ni mabingwa watetezi wa ligi kwa msimu wa 2024/25.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.