KAMATA REKODI ZA MASTAA WA YANGA DHIDI YA SIMBA

KAZI imekwisha Oktoba 19 2024 kwenye Kariakoo Dabi na mwisho ubao wa Uwanja wa Mkapa ukasoma Simba 0-1 Yanga, pointi tatu mikononi mwa Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi. Hizi hapa rekodi za mastaa wa Yanga ilikuwa namna hii:-

DJIGUI DIARRA

Kipa namba moja wa Yanga alikuwa kwenye ubora wake akicheza mchezo wa 5 mfululizo bila kuruhusu nyavu zake kutikiswa ndani ya dakika 450. Tukirudi kwenye Kariakoo Dabi alikomba dakika 90 na hakufungwa.

Hatari aliokoa zaidi ya mbili kubwa kuliko ni ile dakika ya 5 kutoka kwenye miguu ya Leonel Ateba wa Simba, dakika ya 44, 55, 55, 73. Mguu wenye nguvu ni ule wa kulia alitoa pasi zaidi ya 8 ambazo ziliwafikia walengwa na mguu wa kushoto alitoa pasi zaidi ya tatu.

YAO

Yao alichezewa faulo dakika ya 15, alipiga shuti ambalo lililenga lango dakika ya 41 na alikomba dakika zote 90.

LADACK BOCCA

Beki mwenye spidi uwanjani alikutwa kwenye mtego wa kuotea dakika ya 38 alipiga shuti ambalo lililenga lango dakika ya 26, alichezewa faulo dakika ya 28, 45 alicheza faulo dakika ya 37 alionyeshwa kadi ya njano na mwamuzi Ramadhan Kayoko.

JOB

Dickson Job beki wa kazikazi alikomba dakika 90 aliokoa hatari dakika ya 45 alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 46.

BACCA

Ibrahim Bacca alikuwa na vita yake na mshambuliaji Leonal Ateba ni dakika ya 54 alionyeshwa kadi ya njano alikomba dakika zote 90 licha ya kumpisha Jonas Mkude katika dakika zile 7 za nyongeza.

AUCHO

Khalid Aucho kiungo wa kati alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 78 alicheza faulo pia dakika ya 62 na alikomba dakika zote 90.

MAXI

Maxi Nzengeli alikuwa na code za Mnyama alikomba dakika 90 alifunga bao dakika ya 86, alipiga kona dakika ya 69 na alikosa nafasi ya kufunga dakika ya 22.

MUDATHIR YAHYA

Mudathir Yahya alicheza faulo dakika ya 30, 71 alichezewa faulo dakika ya 27, 31, 44 alipiga shuti ambalo lililenga lango dakika ya 78 alikomba dakika 90 licha ya kumpisha Nondo katika dakika 7 za nyongeza.

PRINCE DUBE

Prince Dube alichezewa faulo dakika ya 51, alicheza faulo dakika ya 3, 34, 45 alikutwa kwenye mtego wa kuotea dakika ya 24 alipiga shuti lililolenga lango dakika ya 56 alikomba dakika 61 nafasi yake ilichukuliwa na Clement Mzize.

AZIZ KI

Kiungo Aziz Ki, alichezewa faulo dakika ya 12, 20, 23 alikutwa kwenye mtego wa kuotea dakika ya 11 alipiga kona dakika ya 28, alicheza faulo dakika ya 43, alipiga shuti ambalo halikulenga lango dakika ya 59 alikomba dakika 84 nafasi yake ikachukuliwa na Clatous Chama aliyepiga faulo dakika ya 86.

PACOME

Kiungo Pacome alikomba dakika 62 nafasi yake ilichukuliwa na Kennedy Musonda. Pacome alicheza faulo dakika ya 34, alichezewa faulo dakika ya 17 alipiga shuti ambalo lililenga lango dakika ya 41.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.