HIZI HAPA REKODI ZA MASTAA WA SIMBA KARIAKOO DABI

WAZEE wa Ubaya Ubwela, Simba walipoteza katika mchezo wa Kariakoo Dabi uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Oktoba 19 2024 kwa kushuhudia ubao ukisoma Simba 0-1 Yanga. Ipo wazi kuwa mchezo ulikuwa na ushindani mkubwa kwa kila timu na hapa tunakuletea rekodi za mastaa wa Simba namna hii:-

Mussa Camara

Alianza kikosi cha kwanza chini ya Kocha Mkuu, Fadlu Davids alikomba dakika zote 90 kwenye kuokoa mguu wake wenye nguvu ulikuwa ni ule wa kulia ambao ulipiga zaidi ya pasi 12. Pasi zake kwa asilimia kubwa zilikuwa zikiwafikia walengwa na alitumia mguu wa kushoto kutoa pasi zaidi ya tatu.

Katika kutimiza majukumu yake aliokoa hatari zaidi ya nne licha ya kufungwa bao moja dakika ya 86 na Maxi Nzengeli. Miongoni mwa hatari ambazo aliokoa ilikuwa dakika ya 41, 54, 56, 70, 71 hii ilitokana na pasi fupi aliyompa beki wake wakati anataka kupiga pasi akateleza, hivyo ilimlazimu kuifuata na kuokoa, dakika ya 73.

SHOMARI KAPOMBE

Legend kwenye ubora uleule wa siku zote, hakuwa na mambo mengi utulivu katika kuokoa hatari na kupiga krosi. Miongoni mwa krosi aliyopiga ilikuwa dakika ya 60.

MOHAMED HUSSEN ZIMBWE JR

Nahodha kwenye majukumu yake, ubora uleule kazini alikuwa anapanda na kushuka aliokoa hatari ikiwa ni pamoja na dakika ya 18, 61 alipewa majukumu ya kupiga faulo ilikuwa dakika ya 55 alichezewa faulo dakika ya 80 na alikomba dakika zote 90.

ABDLUAZAK HAMZA

Alianza kikosi cha kwanza alicheza faulo dakika ya 20, 50 alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 50, alipiga shuti ambalo halikulenga lango dakika ya 37 hakusepa na dakika 90 alipata maumivu na dakika ya 68 Chamou aliingia kuchukua mikoba yake.

CHE MALONE

Safu ya ulinzi ilikuwa inaongwa na Che Malone aliokoa hatari zaidi ya mbili na miongoni mwa hizo ilikuwa dakika ya 43, 59, 64 alikomba dakika zote 90.

KAGOMA YUSUPH

Kiungo Yusuph Kagoma alichezewa faulo dakika ya 4, 28, licheza faulo dakika ya 17 alikwama kukomba dakika 90 aligotea dakika ya 45 nafasi yake ilichukuliwa na Okejapha.

KIBU DENNIS

KIBU Dennis anaingia kwenye orodha ya mchezaji aliyechezewa faulo nyingi zaidi Kariakoo Dabi, Oktoba 19 2024.

Miongoni mwa hizo ilikuwa dakika ya 8, 30, 45, 46 alikutwa katika mtego wa kuotea dakika ya 9, 49 alicheza faulo dakika ya 13, 15 na alisababisha kadi ya njano moja kwa Dickson Job dakika ya 46 alikomba dakika 81 akaingia Kelvin Kijili.

MAVAMBO

Mavambo alicheza faulo dakika ya 23, 31, 44 na alichezewa faulo dakika ya 34 alikomba dakika 90 kwenye ubora wake.

ATEBA

Leonel Ateba mshambuliaji wa Simba alikomba dakika 90 alikosa nafasi ya kufunga dakika ya 5 iliyookolewa na kipa Djigui Diarra, alikutwa kwenye mtego wa kuotea dakika ya 16 alichezewa faulo dakika ya 62, 71.

AHOUA

Jean Ahoa kiungo mshambuliaji wa Simba alikomba dakika 90, alicheza faulo dakika ya 12, 45 alionyeshwa kadi ya njano. Alichezewa faulo dakika ya 27, 36, 54, 78 alipiga faulo dakika ya 2, 36, 37, 48, 73.

JOSHUA MUTALE

Kiungo Mutale alipewa majukumu ya kupiga kona ilikuwa dakika ya 49, 50, 56, 57 alikomba dakika 68 nafasi yake ilichukuliwa na Edwin Balua.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.