SIMBA YAPOTEZA KARIAKOO DABI NYUMBANI

SIMBA inayonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids imepoteza mchezo wa Kariakoo Dabi Uwanja wa Mkapa kwa kushuhudia ubao ukisoma Simba 0-1 Yanga.

Bao pekee la ushindi kwa Yanga limefungwa na Maxi Nzengeli dakika ya 86 akitumia makosa ya kipa wa Simba Mussa Camara kutema faulo iliyopigwa na Clatous Chama.

Simba walikosa utulivu kipindi cha kwanza ambapo walitengeneza nafasi mbili kupitia kwa Leonal Ateba ambaye ni mshambuliaji na mwisho wakapoteza.

Kuumia kwa Abdulazack Hamza, Yusuph Kagoma kuliwavuruga Simba kwenye ulinzi huku Yanga ikiwa imara hasa kipindi cha pili na kukomba pointi tatu za Simba ikiwa ugenini.

Yanga inashinda mechi tano mfululizo na kufikisha pointi 15 Simba inasalia na pointi 13 ikiwa imecheza mechi sita, ushindi mechi nne, sare moja na kupoteza mechi moja.

USIPANGE kukosa nakala ya kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo. Mtunzi Lunyamadzo Mlyuka, 0756 028 371.