MWAMBA HUYU HAPA MKALI WA PASI JANGWANI

ZIKIWA zimesalia saa chache kabla ya mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba na Yanga kuchezwa Uwanja wa Mkapa kuna balaa kubwa eneo la kiungo ambapo yupo mtaalamu wa pasi za mwisho ndani ya kikosi hicho kinacholewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi.

Uwanja wa Mkapa kwa sasa mashabiki waliopo nje wanapambana kujikinga na mvua huku wakitafuta nafasi ya kuingia uwanjani kushuhudia mchezo huo wa mzunguko wa kwanza msimu wa 2024/25 unaotarajiwa kuanza saa 11: oo.

Kwenye upande wa pasi za mwisho kutoka kikosi cha Yanga mkali wao ni Aziz Ki ambaye msimu wa 2023/24 aliibuka na tuzo ya ufungaji bora alipofunga mabao 21 kwenye ligi.

Aziz Ki ni namba moja katika watengeneza pasi za mwisho Yanga akiwa katoa pasi tatu na kufunga bao moja ilikuwa kwenye mchezo dhidi ya Pamba Jiji uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.

Nyota huyo chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Miguel Gamondi ni dakika 322 amecheza na kuhusika katika mabao manne yaliyofungwa na Yanga kati ya 8 yaliyofungwa na timu hiyo yenye pointi 12 kibindoni.

USIPANGE kukosa kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ambacho kipo mtaani nakala yake itakufundisha mengi kuhusu maisha ya Kiafrika, kukipata 0756 028 371. Mtunzi Lunyamadzo Mlyuka.