MKALI WA PASI ZA MWISHO BONGO ATUMA UJUMBE HUU

MKALI wa pasi za mwisho Bongo ambaye yupo ndani ya kikosi cha Simba kwa sasa amebainisha kuwa wapo tayari kwa mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa na mwamuzi akiwa ni Ramadhan Kayoko.

Kwenye kutoa pasi za mwisho ndani ya Simba ni kiungo Jean Ahoua ambaye katoa pasi nne za mabao na kufunga mabao mawili kwenye mechi za ligi ambazo alipata nafasi ya kucheza. Amekomba dakika 381 ndani ya ligi akicheza mechi tano ni nguzo katika eneo la kiungo mshambuliaji.

Ahoua amesema kuwa anatambua mchezo wa Kariakoo Dabi sio mwepesi kulingana na ushindani ulivyo lakini malengo yao ni kuona kwamba wanapata ushindi katika mchezo baada ya dakika 90 kwa kuwa pointi tatu ni muhimu.

“Sio mchezo mwepesi ukizingatia ni Kariakoo Dabi ambacho tunahitaji ni kuona kwamba kwa ushirikiano wetu wachezaji na benchi la ufundi tunapata ushindi ili kupata pointi tatu muhimu. Tunaamini inawezekana na tupo tayari.”

Simba baada ya kucheza mechi tano ni ushindi kwenye mechi nne na sare mchezo mmoja. Safu ya ushambuliaji imefunga jumla ya mabao 12 na kukusanya jumla ya pointi 13 kibindoni.

KITABU cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo kipo tayari jipatie nakala yako sasa, oda kupitia 0756 028 371. Posta mkabala na sanamu la askari ukiwa unaelekea IFM kuna wauza vitabu wapo pale nakala zipo, mtunzi Lunyamadzo Mlyuka.