AGGY SIMBA HANA UHAKIKA SIMBA KUWA BINGWA – ”SAJILI NYINGI ZILIKUWA MBOVU BAADA ya MO KUONDOKA” – VIDEO

Shabiki wa klabu ya Simba, Aggy Simba amefunguka kupitia Global TV na kueleza kuwa mashabiki wa klabu ya Simba SC wamechoka kupoteza mbele ya watani zao.

Aggy ameelezea zaidi kuwa kuelekea mchezo dhidi ya Yanga SC wanahitaji ushindi, ikumbukwe mchezo wa dabi ya Kariakoo utachezwa Oktoba 19, 2024 katika dimba la Benjamin Mkapa saa 11:00 jioni.