SIMBA YAPOTEZA KARIAKOO DABI NYUMBANI
SIMBA inayonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids imepoteza mchezo wa Kariakoo Dabi Uwanja wa Mkapa kwa kushuhudia ubao ukisoma Simba 0-1 Yanga. Bao pekee la ushindi kwa Yanga limefungwa na Maxi Nzengeli dakika ya 86 akitumia makosa ya kipa wa Simba Mussa Camara kutema faulo iliyopigwa na Clatous Chama. Simba walikosa utulivu kipindi cha kwanza…