YANGA YASAHAU YALIYOPITA, KUINGIA KWA MPANGO KUIKABILI SIMBA

MIGUEL Gamondi, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa amesahau matokeo yote yaliyopita hivyo kikubwa ni kusaka ushindi kwenye mchezo wa keso ambao ni Kariakoo Dabi, Uwanja wa Mkapa.

Ikumbukwe kwamba msimu wa 2023/24 kwenye Kariakoo Dabi, Yanga ilikomba pointi sita mazima ndani ya dakika 180 kwa kushinda nje ndani.

Oktoba 19 2024 historia inakwenda kuandikwa kwa watani hao wa jadi kukutana uwanjani kusaka pointi tatu kwa timu zote mbili ndani ya dakika 90 ikiwa ni mzunguko wa kwanza.

Gamondi amesema: ” Tunawaheshimu wapinzani wote tunaocheza nao ligi kuu. Ni kweli kesho tuna mechi ngumu kwani ni Derby, lakini tunajua namna tunauendea mchezo. Kila mara nasema mimi huwa sitazami sana historia. Yaliyopita yamepita, malengo yetu ni kutazama yanayokuja mbele yetu.

“Tumetokea kwenye wiki ya FIFA na mara nyingi tunapata changamoto kidogo ya maandalizi kwani wachezaji wetu wengi wanakuwa kwenye majukumu ya timu za TAIFA. Kwa mfano kuna wachezaji wamefika jana na wengine wanaingia leo kwa mantiki hiyo lazima upate ugumu kwenye maandalizi lakini tutafanya kila liwezekanalo.”

Yanga ambao ni mabingwa watetezi wa ligi baada ya kucheza jumla ya mechi nne wameshinda zote na kukomba pointi 12 kibindoni.

USIPANGE kukosa nakala yako ya kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, hii ni hadithi ambayo inazungumzia maisha ya Kiafrika, Usaliti, Visasi hakika hautajuta kupata nakala yako. Wakazi wa Njombe tayari kitabu kimefika mtaa wa Mpechi, kukipata 0756 028 371.