SIMBA: SIKU HAZIGANDI, TUNAWATAKA NYUMA MWIKO

NI Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba ameweka wazi kuwa siku hazigandi na wanaamini watakutana na wapinzani wao Yanga kwenye mchezo wa Kariakoo Dabi Oktoba 19 2024 Uwanja wa Mkapa.

Ikumbukwe kwamba kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii hatua ya nusu fainali Uwanja wa Mkapa baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba 0-1 Yanga bao la ushindi likifungwa na Maxi Nzengeli ambaye amekuwa kwenye ubora wake ndani ya uwanja.

Saa zinahesibika kabla ya mchezo huo kuchezwa kwa wababe hao wawili kusaka pointi tatu muhimu huku Ally akiweka wazi kuwa wanatambua wanachohitaji kwenye mchezo huo ni ushindi.

“Kwenye mchezo wetu dhidi ya nyuma mwiko ambacho tunahitaji ni ushindi hiyo Oktoba 19 2024, wanasema siku zinakimbia hilo lipo wazi na siku hazigandi hivyo tutakutana uwanjani kwa ajili ya msako wa pointi tatu.

“Hatukuwa na matokeo mazuri dhidi yao kwenye mechi zetu ambazo zilipita hivyo hilo halitabadilika lakini kwenye mechi ambayo ipo mbele yetu sasa tunahitaji kupata ushindi muhimu na wachezaji wetu wote wapo kamili.”

USIPANGE kukosa nakala ya kitabu cha hadithi kinachoitwa Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ambacho kinazungumzia masuala ya maisha ya Kiafrika, usaliti, visasi. Kukipata 0756 028 371.