MASTA GAMONDI REKODI ZAKE HIZI HAPA

KUELEKEA Kariakoo Dabi, Oktoba 19 2024 kila timu imekuwa ikipambana kufanya maandalizi na saa zinahesabika kwa sasa kujua nani atakuwa nani baada ya dakika 90 kugota mwisho.

Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi baada ya kucheza mechi nne ambazo ni dakika 360 imekomba ushindi mechi zote nne za Ligi Kuu Bara. Kwenye msako wa pointi 12 zote zimewekwa kibindoni mazima kwa mabingwa hao watetezi wa ligi. Safu ya ushambuliaji ya Yanga imefunga mabao 8 na ukuta haujaruhusu kufungwa ndani ya uwanja katika mechi za ushindani.

Kinara wa utupiaji ni kiungo Maxi Nzengeli ambaye yeye katupia jumla ya mabao matatu kwenye mechi nne ambazo Yanga imecheza ndani ya uwanja kwenye msako wa ushindi.

HIZI HAPA ZA GAMONDI

Kagera Sugar 0-2 Yanga mchezo huu ulichezwa Uwanja wa Kaitaba, Agosti 29 2024 na mtupiaji wa bao la kwanza ni Maxi Nzengeli ndani ya Yanga kwenye ligi.

Ken Gold 0-1 Yanga huu ulikuwa mchezo wa pili kwa Yanga ugenini ilikuwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya mtupiaji alikuwa ni Ibrahim Bacca ambaye alitumia pasi ya Aziz Ki Septemba 25 2024. Yanga 1-0 KMC, mchezo wa kwanza wakiwa Uwanja wa Azam Complex msimu wa 2024/25 ilikuwa Septemba 29 2024.

Yanga 4-0 Pamba Jiji ushindi mkubwa kwa Yanga ndani ya 2024/25 walikuwa Azam Complex  ilikuwa Oktoba 3 2024 kituo kinachofuata ni Oktoba 19 dhidi ya Simba.

USIKOSE kupata nakala ya kitabu cha Hadithi kinachoitwa Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, Mtunzi Lunyamadzo Mlyuka, kitabu hicho kimezungumzia masuala ya maisha, mikasa ya usaliti na kazi. Kukipata 0756 028 371.