>

RAIS WA KLABU YA BIASHARA UNITED YA MARA, REVOCATUS GABRIEL RUGUMILA AJIPA ‘THANK YOU’

Aliyekuwa Rais wa klabu ya Biashara United ya Mara, Revocatus Gabriel Rugumila ameamua kuachana na timu hiyo kuanzia tarehe 10/10/2024 kutokana na makubaliano ya uendeshaji kwa timu hiyo.

Taarifa ya idara ya habari na mawasiliano ya klabu hiyo iliyotolewa Oktoba 11, 2024 imebainisha kuwa uamuzi huo umezingatia makubaliano yaliyopo kwenye mkataba wa uendeshaji wa timu baina yake na Wanachama waanzilishi wa Biashara United huku timu hiyo ikisalia chini ya uangalizi wa Mwenyekiti wa Wanachama waanzilishi.