>

ARSENAL NAO SIO HABA WANAENDELEA WALIPOISHIA

Klabu ya Arsenal wameonekana kuuanza msimu huu kama ambavyo walimaliza msimu uliomalizika kwani klabu hiyo ni moja ya vilabu ambavyo vinafanya vizuri kunako ligi kuu ya Uingereza wakikamata nafasi tatu kwenye msimamo.

 

Arsenal mpaka sasa hawafanikiwa kupoteza mchezo hata mmoja kunako ligi kuu ya Uingereza kwenye michezo saba ambayo klabu hiyo imecheza, Kwani mpaka sasa wameshinda michezo mitano na kusare michezo miwili.

 

Vijana wa Mikel Arteta wamejikusanyia alama 17 mpaka sasa wakidondosha alama 4 mpaka sasa kati ya alama 21 ambazo walitakiwa wakusanye kwenye michezo saba, Huku ikionekana sio wastani mbaya mpaka sasa.

 

Kitu cha tofauti kwa klabu hiyo mpaka sasa ni kua ilizoeleka misimu miwili nyuma kua kipindi kama hiki wanakua wanaongoza msimamo wa ligi kuu ya Uingereza, Lakini msimu huu wanakamata nafasi ya tatu wakati huu ligi zimesimama kupisha michuano ya kimataifa lakini hata hivo hawako mbali na vinara wa ligi hiyo klabu ya Liverpool.

 

Endelea kufurahia kubashiri na Meridianbet mabingwa wa michezo ya kubashiri ambao wanatoa ODDS BOMBA kuliko mahala pengine, Lakini pia machaguzi mengi zaidi ya 1000 Bashiri sasa michezo itakayopigwa wikiendi hii uweze kupiga mkwanja.

 

Washika mitutu kutoka jiji la London bado inaonekana ni timu ambayo inautaka ubingwa kwa udi na uvumba, Kwani bado wana kikosi cha ushindani ambacho kinaweza kupata matokeo dhidi ya timu yeyote lakini pia wana faida ya kikosi ambacho kimekaa kwa muda mrefu pamoja na kutengeneza muunganiko mzuri.