>

HAWA HAPA WAPINZANI WA SIMBA KIMATAIFA

DROO ya Kombe la Shirikisho imepangwa nchini Misri ambapo wawakilishi kwenye anga hilo kutoka Tanzania ni Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids.

Simba imepangwa kundi A na ilikuwa POT 1 lililokuwa na Zamalek, RS Berkane, Simba, USM Alger ambazo hizi hazitakuwa pamoja kwenye makundi na POT 2 lilikuwa na ASEC Mimosas, Stade Malien, Al Masry na CS Sfaxine,  POT 3 lilikuwa na Enyimba, ASC Jaraaf ambazo hizi hazitakutana.

Makundi yapo namna hii:-

KUNDI A

Simba
CS Sfaxien
CS Constantine
FC Bravos do Maquis

KUNDI B
RS Berkane
Stade Malien
Stellenbosch
CD Luanda

KUNDI C
USM Alger
ASEC Mimosas
ASC Jaraaf
Orapa United

KUNDI D
Zamalek SC
Al Masry
Enyimba FC
Black Bulls

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kuipata 0756 028 371