>

BACCA ANATAKA KUFUNGA KILA MECHI

BEKI wa kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi Ibrahim Bacca amesema kuwa mpango mkubwa ni kuona kwamba anafunga kila mechi.

Nyota huyo alifungua akaunti ya mabao kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ken Gold uliochezwa Uwanja wa Sokoine akitumia pasi ya Aziz Ki ambaye kwenye mchezo huo alipiga faulo nje kidogo ya 18 akitumia mguu wa kushoto.

Baada ya mchezo huo Bacca kwenye mahijiano na Waandishi wa Habari aliporejea Dar alibainisha kwamba anahitaji kutwaa tuzo ya ufungaji bora msimu wa 2024/25.

Ikumbukwa kwamba tuzo ya ufungaji bora ipo mikononi mwa Aziz Ki ambaye msimu wa 2023/24 alitupia mabao 21 kibindoni ndani ya ligi na Yanga ilitwaa ubingwa.

Mchezo wa pili Bacca kufunga ilikuwa dhidi ya Pamba Jiji uliochezwa Uwanja wa Azam Complex baada ya dakika 90 Yanga ilishinda mabao 4-0 na kukomba pointi tatu muhimu.

Bacca amesema: “Ninapenda kufunga na ninahitaji kuona kwamba kila mechi ambazo tunacheza ninafunga na yote haya yanatokana na ahadi niliyotoa ya kutaka kuwa mfungaji bora.”

Kituo kinachofuata kwa Yanga ni Oktoba 19 2024 Kariakoo Dabi itakuwa dhidi ya Simba mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi wa Kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata 0746 028 371.