SIMBA: UBAYA UBWELA UMEANZA KUFANYA KAZI

UONGOZI wa Simba umebainisha kuwa tayari ubaya ubwela umeanza kufanya kazi kwa vitendo jambo linalofanya wapinzani wao kuanza kutapatata kwenye mechi ambazo haziwahusu kwa namna yoyote ile.

Simba baada ya kucheza mechi nne za ligi imekomba 12 ikipata ushindi kwenye mechi zote ambazo ilicheza huku safu ya ushambuliaji ikiwa imetupia mabao 10 ikiwa namba mbili kwa timu zenye safu kali ya ushambuliaji kinara ni Fountain Gate ni mabao 12 imefunga baada ya kucheza jumla ya mechi 6.

Septemba 30 Simba ilimtambulishwa mwamba Mpanzu Elie Nkibisawala kuwa ingizo jipya ndani ya kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu Fadlu Davids.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa wanatambua namna hali ilivyo kwenye mechi wanazocheza na matokeo kuwashangaza wengine huo ni ubaya ubwela unafanya kazi.

“Ubaya ubwela umeanza kufanya kazi tunapata ushindi sisi uwanjani kisha wao wanaanza kujadili kelele zinakuwa nyingi kweli hili linaonekana hivyo wataendelea kusema kila siku sisi tunapambania kupata pointi tatu muhimu.

“Sasa tulikuwa tunawaambia kuhusu ubaya ubwela wakabadilisha wakaita ubaya ubwege tukachuna wakasema hakuna kitu kwenye mechi za mwanzo, tukaanza kushinda ohh wanashinda kwa timu ndogo sasa tumeshinda kwenye mechi zetu nne pongezi kwa wachezaji wao waendelee ubaya ubwela sasa upo kwa vitendo.”

Simba ni nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi baada ya kucheza mechi nne vinara ni Singida Black Stars baada ya kucheza mechi 5 wamekusanya pointi 13 kibindoni.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kuipata 0756 028 371