KMC KUIMARISHA SAFU YA USHAMBULIAJI

KOCHA Mkuu wa KMC Abdihamid Moalin amesema kuwa watafanya kazi kubwa kwenye kuimarisha safu ya ushambuliaji ili kuwa bora kwenye mechi ambazo wanacheza za ushindani ndani ya Ligi Kuu Bara.

KMC mchezo wake uliopita ilikuwa ugenini baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Azam Complex ulisoma Yanga 1-0 KMC bao la ushindi lilifungwa na Maxi Nzengeli dakika ya 4 lilidumu mpaka mwisho wa mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa.

Akizungumza na Saleh Jembe, Moalin amesema kuwa wamekuwa wakipata nafasi kwenye mechi ambazo wanacheza lakini kuzitumia imekuwa ngumu jambo ambalo wanalifanyia kazi.

“Unaona kwenye mechi zetu ambazo tunacheza tumekuwa tukipata nafasi nyingi lakini kuzibadili kuwa bao hapo kumekuwa na tatizo huo ni ukweli kwa kuwa mchezo wa mpira ni mchezo wa wazi na ninazungumza na wachezaji kuona kwamba tunakuwa bora zaidi.

“Mchezo uliopita ilikuwa dhidi ya Yanga tulikuwa tumejipanga kuwakabili wapinzani wetu mwisho tukapoteza mchezo ule ambacho kimetokea ni matokeo huwezi kubadili hivyo muhimu ni kuona kwamba mechi zijazo tunafanya vizuri na kupata matokeo uwanjani.”

KMC baada ya kucheza jumla ya mechi sita ndani ya uwanja ambazo ni dakika 540 safu yake ya ushambuliaji imefunga jumla ya mabao matatu ndani ya uwanja ikiwa na wastani wa kufunga bao moja kila baada ya dakika 180.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata 0756 028 371