>

SINGIDA BLACK STARS BADO NAMBA MOJA

SINGIDA Black Stars wamerejea kwa mara nyingine namba moja kwa kuishusha Fountain Gate ambayo iliweka kambi hapo kwa muda ilipopata ushindi kwenye mchezo wake uliopita dhidi ya Kagera Sugar.

Sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya JKT Tanzania inawafanya wafikishe pointi 13 kibindoni kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ambao ushindani wake ni mkubwa.

Katika mchezo uliochezwa Septemba 29 ni Elvis Rupia alianza kufunga kwa Singida Black Stars dakika ya 15 bao hilo lilikwekwa usawa na Wilson Nangu dakika ya 65.

Hivyo wakiwa nyumbani Uwanja wa Liti wamepata sare ya kwanza ndani ya msimu wa 2024/25 kwa kuwa mechi nne za mwanzo zote waliambulia ushindi na kufikisha jumla ya pointi 13 kibindoni.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo,kuipata 0756 028 371.