>

KMC: TUNA HASIRA KUPOTEZA MBELE YA YANGA

UONGOZI wa KMC umeweka wazi kuwa una hasira kupoteza mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga hivyo hesabu kubwa ni kufanya vizuri kwenye mechi zijazo.

Katika mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Azam Complex, Septemba 29 baada ya dakika 90 ubao ulisoma Yanga 1-0 KMC na bao la ushindi lilifungwa na Maxi Nzengeli dakika ya nne.

Khalid Chukuchuku, Ofisa Habari wa KMC ameweka wazi kuwa walikuwa na mpango mkubwa wa kupata pointi tatu kwenye mchezo huo bahati haikuwa upande wao kutokana na wapinzani wao kupata bao la mapema.

“Kwenye mchezo wetu dhidi ya Yanga Uwanja wa Azm Complex wachezaji walifanya kazi kubwa kutafuta ushindi lakini bahati haikuwa upande wetu hilo limetupa hasira kwenye mchezo wetu ujao tunaamini tutafanya vizuri kupata pointi tatu kwa kuwa tuna hasira za kupoteza mchezo wetu uliopita.

“Kila mmoja anatambua namna ambavyo wachezaji walicheza na bao la mapema walilopata wapinzani wetu ukiangalia mazingira yake utaona kwamba kulikuwa na makosa madogo ambayo yakifanyiwa kazi tutakuwa imara zaidi.”

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata 0756 028 371.