>

GANZI YA MAUMIVU KUWAFIKIA WAKAZI WA NJOMBE

HATIMAYE ile simulizi ya Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo iliyopata nafasi ya kutoka kwenye gazeti la Championi na kusomwa na zaidi ya Watanzania milioni sasa inakwenda kuwafikia wakazi wa Njombe na vitongoji vyake hivi karibuni.

Ikumbukwe kwamba hii ni simulizi ya kwanza kuwa kwenye mfumo wa kitabu imeandikwa na Mtunzi Lunyamadzo Myuka, A Boy From Njombe ipo tayari mtaani ikianza kupatikana kwa wakazi wa Dar na vitongoji vyake.

Wakazi wa Sinza Mori, Mbangala, Kigamboni, Goba, Sinza Kumekucha tayari wameanza kupata nakala zao ambapo namba ya oda ni 0756 028 371 hapo ulipo inakufikia na unaweza kufika pia makao makuu ya Global Group Sinza Mori kapata kitabu cha Lunyamadzo pamoja na vitabu vya Legendi kwenye utunzi wa hadithi Eric Shigongo.

Mpango kazi uliopo kwa sasa ni nakala kuwafikia wakazi wa Njombe baada ya maombi ya wengi kufanyiwa kazi hivyo ni muda wa wakazi wa Njombe na Vitongoji vyake kukaa mkao wa kuisoma simulizi hiyo ambayo imekuwa gumzo kwa sasa.

Simulizi hiyo inazungumzia maisha halisi ya Kiafrika huku ikitoa somo kuhusu atahari za madawa ya kulevya, athari za makundi.

Hii ni kwa ajili yako hakika ukiipata nakala hii hautajuta utarudi kunishukuru baadaye. Imehaririwa na Omary Mdose, Minaj, Mhakiki wa Simulizi hiyo ni Mwandishi Bora mwenye tuzo ya uandishi Bongo Joseph Shaluwa ambaye pia kasimamia kwenye masuala ya chapa ya kwanza ya kitabu hicho na msanifu kurasa ni Bahati Haule.