>

PATACHIMBIKA LEO ZANZIBAR AZAM vs SIMBA

LIGI Kuu ya NBC Tanzania bara inaendelea tena leo Septemba 26, 2024 kwa mchezo mmoja wa Derby ya Mzizima, kati ya wenyeji Azam Fc dhidi ya Wekundu wa Msimbazi Simba Sc utakaopigwa visiwani Zanzibar katika dimba la New Amaan Complex.

Simba Sc itakosa huduma ya nyota wake wawili muhimu, Yusuph Kagoma na Mzamiru Yassin kukotana na majeraha huku Meneja wa Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo Ahmed Ally akisema kukosekana kwa nyota hao ni pengo kubwa lakini Simba ni timu kubwa na ina wachezaji wengi.

Mchezo huo utakaosimamiwa na Mwamuzi Hery Sasii utachezwa majira ya saa 2:30 usiku utakuwa wa tano kwa Azam Fc wenye pointi 8 baada ya mechi nne huku ukiwa mchezo wa tatu kwa Simba Sc wenye alama 6.

Azam Fc imepoteza mara mbili mfululizo kwenye mechi zilizopita dhidi ya Mnyama wakipoteza 3-0 kwenye Ligi mnamo Mei 9, 2024 kwa magoli ya Sadio Kanoute, Fabrice Ngoma na David Kameta β€˜Duchu’ baada ya kupoteza 1-0 kwenye fainali ya kombe la Muungano 2024 kwa bao pekee la Babacar Sarr.

20:30 AZAM Fc vs SIMBA Sc
🏟️ New Amaan Complex, Zanzibar
πŸ†: #NBCPremierLeague

✍️ Nani kuchomoza na pointi tatu muhimu?