>

MZIZIMA DABI LEO, FOUNTAIN GATE MKWARA MZITO

LIGI Kuu Tanzania Bara inaendelea baada ya Septemba 25 2024 mabingwa watetezi wa ligi Yanga kusepa na pointi tatu ugenini dhidi ya Ken Gold, mchezo uliochezwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Bao pekee la ushindi kwenye mchezo huo lilifungwa na Ibrahim Bacca beki wa kazi akitumia pasi ya Aziz Ki ambaye kwenye mechi mbili mfululizo ametoa pasi akikomba jumla ya dakika 169 ndani ya uwanja.

Leo Septemba 26 ni Mzizima Dabi mchezo utakaowakutanisha Azam FC dhidi ya Simba unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa New Amaan Complex.

Septemba 27 Ligi Kuu Bara itakuwa kazini ikicheza dhidi ya Kagera Sugar, itakuwa Uwanja wa Kwaraa, Tanzanite saa 10;00 jioni.

Issa Liponda, Ofisa Habari wa Fountain Gate amesema kuwa wapo tayari kwa mchezo huo wapo tayari kwa mchezo huo na kikubwa ni kupata pointi tatu muhimu.

“Tayari kikosi kipo tayari kwa mchezo wetu dhidi ya Kagera Sugar na maandalizi yapo tayar hivyo kwa namna yoyote ilepointi tatu zitabaki hapa na tutagawana sukari baada ya kumaliza kukamua kwenye mchezo wetu wa dakika 90 za kazi.”

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata 0756 028 371.