LIGI Kuu Tanzania Bara inaendelea ikiwa ni mzunguko wa kwanza msimu wa 2024/25 ambapo kila timu zipo tayari kwenye msako wa pointi tatu muhimu.
Vinara ni Singida Black Stars baada ya kucheza mechi nne wamekomba pointi zote 12 huku nafasi ya pili ikiwa ni Fountain Gate yenye pointi 10, Ken Gold ambayo itakuwa kazini leo baada ya kucheza mechi nne haijakusanya pointi.
Ratiba ipo namna hii Septemba 25 2024:-
Saa 8:00 mchana, JKT Tanzania watakuwa uwanja wa nyumbani Meja Jeneral Isamuhyo wakiwakaribisha Coastal Union.
JKT Tanzania ipo nafasi ya 13 ina pointi tatu baada ya kucheza mechi tatu zote ikiambulia pointi mojamoja na Coastal Union baada ya kucheza mechi 4 imekusanya pointi moja nafasi ya 15.
JKT na Coastal wote hawajapata ushindi tangu msimu uanze na mchezo uliopita Coastal Union ikiwa ugenini ilishuhudia ubao wa Uwanja wa Azam Complex ukisoma Azam FC 1-0 Coastal Union.
Saa 10:15 Yanga ambao ni mabingwa watetezi watakuwa ugenini Uwanja wa Sokoine kukipiga na Kengold. Ni mchezo wa pili kwa Yanga kwenye ligi msimu wa 2024/25 mchezo wa kwanza ilikuwa dhidi ya Kagera Sugar uliochezwa Uwanja wa Kaitaba.
Na: Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi wa Kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata 0756 028 371.