MPANZU NI MALI YA SIMBA

WINGA raia wa DR Congo Ellie Mpanzu rasmi amemalizana na Simba kwa kusaini dili la miaka miwili kuitumikia timu hiyo ambayo inanolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids.

Ikumbukwe kwamba Septemba 22 Mpanzu alikuwa Uwanja wa Mkapa kushuhudia timu hiyo ikicheza mchezo wa raundi ya pili Kombe la Shirikisho kusaka mshindi wa kutinga hatua ya makundi na jambo hilo lilifanikiwa ubao uliposoma Simba 3-1 Al Ahli Tripoli ya Libya.

Simba walikuwa wanaiwinda saini ya Mpanzu ambapo walikuwa wanatajwa kumalizana naye kwenye dili la awali ila mambo yalibadilika nyota huyo akapata timu Ulaya mipango ilivyokwama huko akarejea DR Congo na kufufua mazungumzo yake na Simba hatimaye dili lake limekamilika.

Atakuwa ndani ya Simba kwa msimu wa 2024/25 dirisha dogo la usajili litakapofunguliwa kwa kuwa hakuwa kwenye mpango wa mechi za awali msimu wa 2024/25 ambao una ushindani mkubwa.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Dizo Click.