>

AZAM WAPATA USHINDI WA KWANZA WAIPIGA KMC BAO 4-0

LIGI Kuu ya NBC Tanzania bara imeendelea tena leo Septemba 19, 2024 kwa mchezo mmoja ambapo Wanalambalamba, Azam Fc wamepata ushindi wa kwanza wa msimu kufuatia ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya wenyeji, KMC Fc katika dimba la KMC Complex Mwenge, Dar es Salaam.

Mabao wa Waoka Mikate hao yametiwa kimiani na

Idd Bado alikuwa wa kwanza kufunga bao mnamo dakika ya 19 za kipindi cha kwanza na kuwapeleka Waoka Mikate hao mapumzikoni wakiwa mbele 1-0 kabla ya Lusajo Mwaikenda (dk 55), Nassor Saadun (dk 60) na Nathaniel Chilambo (67’) kuongeza mengine na kukamilisha karamu ya magoli 4-0.

Kwa ushindi huo Wanalambalamba wamefikisha pointi 5 baada ya mechi tatu na kukwea mpaka nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi huku KMC Fc wakiteremka mpaka nafasi ya 8 pointi 4 baada ya mechi 4.

FT: KMC FC 0-4 AZAM FC
⚽️ Nado 19’
⚽️ Mwaikenda 55’
⚽️ Saadun 60’
⚽️ Chilambo 67’