NYOTA mpya wa Yanga, Prince Dube ana balaa zito ndani ya kikosi cha Yanga kwenye mechi ambazo anacheza licha ya kushindwa kufunga mabao mengi katika nafasi anazopata huku benchi la ufundi likibainisha kwamba wanasuka upya safu ya ushambuliaji kuongeza makali uwanjani.
Ipo wazi kwamba kuna vita kubwa eneo la ushambuliaji Yanga ikiwa kuna Clement Mzize, Kennedy Musonda hawa wote ni washambuliaji na yupo mwamba aliyekuwa Simba Jean Baleke.
Dube amekuwa na zali la kupata nafasi kwenye mechi anazocheza ikiwa iaonyesha kuwa ni mshambuliaji anayependa kazi yake ikumbukwe kwamba kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar ambao ulikuwa ni mchezo wake wa kwanza akiwa na uzi wa Yanga nafasi zaidi ya tano za wazi alikosa.
Ilikuwa dakika ya 2, 18, 21, 31 mashuti yake yalilenga lango lakini yaliokolewana mlinda mlango Chalamanda wa Kager Sugar hivyo akiongeza umakini kuna balaa zito linakuja.
Kwenye mchezo wa kimataifa wa Ligi ya MabingwaAfrika dhidi ya CBE SA Dube alifunga bao pekee la ushindi dakika ya 45 wakiwa ugenini licha ya kukosa nafasi zaidi ya mbili anazidi kuimarika taratibu.
Mchezo ujao wa marudiano unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa New Amaan Complex, Septemba 21 ambapo mshindi wa jumla kwenye mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Afrika atatinga hatua ya makundi.
Miguel Gamondi, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa alizungumza na wachezaji wake wote ikiwa ni pamoja na Dube ili kuwa imara kwenye mechi zinazofuata kwa kuwa ni ngumu kutengeneza nafasi nyingi katika mechi za kimataifa.
“Tunakwenda kufanyia kazi makosa ambayo yalipita kwa kuja na mpango mpya kikubwa ni kuona matokeo yanapatikana kumbuka kwamba ni ngumu kutengeneza nafasi nyingi kwenye mechi za kimataifa kikubwa ni kuona kwamba tunapata ushindi.”