KAMPUNI mpya ya kimataifa ya michezo ya kubashiri ya mitandaoni na kwenye Kasino ya LEONBET imeingia rasmi katika soko la Tanzania.
Kampuni hiyo ambayo inafanya shughuli zake katika nchi 19 duniani kote, tayari imepewa leseni ya kufanya shughuli zake nchini na Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT).
Mkurugenzi Mkuu wa LEONBET Tanzania, Tumaini Maligana anathibitisha wamepewa namba ya usajili SBI000000051 kwa ajili ya kuendesha michezo ya kubashiri ya mitandaoni na OCL00000027 kwa ajili ya kufanya shughuli za michezo ya Kasino.
Maligana alisema kuwa LEONBET inatoa huduma za kisasa zaidi na hiyo ndiyo sababu kubwa ya kupanua wigo na kuingia katika soko la Tanzania.
“LEONBET inalenga kuleta mapinduzi katika tasnia ya michezo ya kubashiri mtandaoni na kwenye kasino. Imejidhatiti kutoa huduma bora zaidi, uwepo wa kipekee mtandaoni, na bonasi zinazovutia ili kuhakikisha kuwa wateja wetu wanapata thamani halisi ya pesa zao.
Kampuni hii ni ya kisasa zaidi na imejipanga kwa kukabiliana na ushindani wa michezo ya kubashiri ya mitandaoni na kwenye Kasino kama tulivofanya katika nchi nyingine 19 duniani,” alisema Maligana.
Alisema kuwa kwa zaidi ya miaka 15, LEONBET imekuwa ikitoa huduma bora za kubashiri michezo a mitandaoni na ya Kasino kwa wateja wake na kuwavutia wengi.
“LEONBET ipo tayari kuleta burudani hiyo kwa Watanzania wote. Kwa kutumia simu ya mkononi, kompyuta, au Ipad, unaweza kubeti kwenye michezo mbalimbali. Sloti zetu ni za kuvutia, pia tuna michezo kibao ya kasino mtandaoni. Tumekuja kivingine kabisa na tunawahakikishia wateja wetu malipo fasta, usajili rahisi, bonus za kibabe, odds kubwa, huduma masaa 24,” alisema Maligana.
Alifafanua kuwa LEONBET imeleta huduma rahisi na bora kwa wateja wa Tanzania na usajili wake ni rahisi sana.
“Ili kujisajili, unatakiwa kuwa na namba ya simu na neno la siri lako tu. Pia tunatoa njia rahisi za kuweka pesa na malipo ya haraka kupitia mitandao yote ya simu nchini. Huduma zetu kwa wateja zinapatikana kwa masaa 24 kila siku na kukuwezesha kupata msaada wakati wowote unapohitaji,” alisema.
Kwa mujibu wa Malingana, mteja yeyote atakayejisajili na kuwa sehemu ya familia ya LEONBET, unapata Sh2,000 bure kama ofa maalumu ya kujiunga, ambayo utaendelea kuipata kila unapoingia hadi mara nne kwa mwezi wa kwanza.
“Ofa hii inakuwezesha kuanza safari yako ya ushindi bure kabisa. Kwa upande wa michezo ya kasino, unapata bonasi ya ukaribisho ya asilimia 40 hadi Sh4 milioni, iliyogawanywa mara nne, kila moja ikiwa na bonasi ya asilimia 100 hadi Sh1,000,000. Tunaomba kila mteja achangamkie ofa hii ya kibabe, asikubali impite, jiunge na LEONBET Leo, jiunge na Chimbo Jipya la Washindi. Naomba wateja wetu wafuatilie zaidi kwenye mitandao yetu ya kijamii ili kupata maelezo ya kina zaidi,” alisisitiza.