YANGA YASHINDA UGENINI, TATIZO LIPO HAPA

WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika Yanga karata yao ya kwanza katika hatua ya pili wameibuka na ushindi ugenini kwenye mchezo wao uliochezwa Ethiopia.

Licha ya timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi kwa kushuhudia ubao ukisoma CBE SA ya Ethiopia 0-1 Yanga bado kuna kazi kubwa ambayo benchi la ufundi litakwenda kufanyia kazi katika eneo la ushambuliaji ili kuwa imara zaidi.

Bao la ushindi limefungwa na Prince Dube dakika ya 45 huku nafasi za wazi zikikoswa na wachezaji ikiwa ni Clement Mzize, Clatous Chama dakika ya 85.

Yanga inarejea Bonngo kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wake ujao wa marudio ili kumpata mshindi wa jumla ambaye atakwenda hatua ya makundi.

Ushindi huo ugenini ni hatua kubwa kwa Yanga kutanguliza mguu mmoja katika hatua inayofuata ambapo kwenye mchezo wa pili kazi yao ni kulindi ushindi na kupata mabao mengi zaidi ili kusonga mbele.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Dizo Click.