YANGA KUWAKABILI WAETHIOPIA KIMKAKATI

WAWAKILISHI wa Tanzania Yanga kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika watakuwa na kazi ya kuwakabili wapinzani wao CBE SA ya Ethiopia leo Septemba 14 2024 huku wakipiga hesabu kuwakabili kimkakati kupata ushindi katika mchezo huo.

Ipo wazi kwamba katika timu mbili ambazo zilianzia hatua ya awali Ligi ya Mabingwa Afrika ni Yanga imesonga mbele baada ya kuwafungashia virago Vital’O  kwa ushindi wa jumla ya mabao 10-0 huku Azam FC ikigotea kwenye hatua ya awali.

Meneja wa Yanga, Walter Harrison amesema kuwa wachezaji wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo ambao utakuwa na ushindani mkubwa kikubwa ni kuona kwamba wanapata matokeo wakiwa ugenini.

Miguel Gamondi, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa wapo tayari kwa mchezo huo na mkakati mkubwa ni kupata matokeo mazuri uwanjani katika mchezo huo muhimu.

“Ni mchezo muhimu kwetu na tunatambua kwamba mechi za Ligi ya Mabingwa hizi mkakati kwa kila timu ni kupata ushindi hilo tunalitambua na tupo tayari kwa ajili ya mchezo wetu. Makosa yaliyopita tumeyafanyia kazi ili kuwa imaa katika mchezo wetu.”

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Abebe nchini Ethiopia wakicheza na CBE SA, saa 9:00 alasiri.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka.