>

SIMBA BADO KUNA TATIZO LA ULINZI LIFANYIWE KAZI

SAFU ya ulinzi ya Simba inayoongozwa na Che Malone bado ni tatizo kutokana na kufanya makosa ya mara kwa mara katika eneo la 18 jambo ambalo litawagharimu wasipolifanyia kazi.

Kumbuka kwamba katika mechi mbili za Ligi Kuu Bara wakitumia dakika 180 safu ya Simba haikufungwa lakini walikutana na timu ambazo hazikufanya mashambulizi mara nyingi zaidi Tabora United na Singida Fountain Gate.

Mchezo dhidi ya Al Hilal ulitoa picha kamili namna eneo la ulinzi lilivyo pamoja na washambuliaji kutokuwa makini kulinda mipira na kukaba pia.

Ikumbukwe kwamba Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally aliweka wazi kuwa kumekuwa na tatizo kwenye eneo la ulinzi kwenye kufanya makosa jambo ambalo litafanyiwa kazi na benchi la ufundi.

“Unaona kwenye mechi zetu ambazo tunacheza licha ya kupata ushindi mechi mbili za ligi bado kumekuwa na tatizo eneo la ulinzi hilo linafanyiwa kazi kwani ili kupata ushindi ni muhimu kuwa na safu imara ya ulinzi, mashabiki wasiwe na mashaka tunaamini hili litafanyiwa kazi.”

Kwenye anga la kimataifa Simba inapeperusha bendera kwenye Kombe la Shirikisho na itakuwa na kibarua ugenini Septemba 15 2024 Al Ahly Tripoli v Simba, saa 2:00 usiku.