>

MASTAA SIMBA NDANI YA MAISHA MAPYA YANGA

MAISHA ya mpira yana kupanda na kushuka ambapo kila mchezaji uwanjani amekuwa na kazi kubwa kuonyesha uwezo wake ndani ya dakika 90 na wapo ambao wamekuwa wakiongezewadili jipya na wengine kukutana na Thank You.

Msimu wa 2023/24 ipo wazi kwamba Yanga ni mabingwa wa ligi chini ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi na sasa wanakibaua kingine kupambania taji hilo ambapo mchezo wa kwanza wa ligi kwa msimu wa 2024/25 waliibuka na ushindi ugenini.

Ipo wazi kwamba baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Kaitaba ulisoma Kagera Sugar 0-2 Yanga na mabao ya Yanga yalifungwa na Maxi Nzengeli dakika ya 25 na Mzize Clement ilikuwa dakika ya 88 akitumia pasi ya Aziz Ki.

Kuna mastaa ndani ya kikosi cha Yanga ambao waliwahi kucheza pamoja ndani ya kikosi cha Simba sasa wote watakuwa kwenye uzi wa njano na kijani wakipambania kombe kwenye changamoto mpya.

Miongoni mwa hao ni pamoja na mshambuliaji Jean Baleke huyu alikutana na Thank You Simba kwenye dirisha dogo la usajili jambo lililoleta mshtuko kwa kuwa wakati huo alikuwa ni kinara kwenye eneo la utupiaji alipofunga mabao 8 kibindoni.

Ikumbukwe kwamba msimu wa 2022/23 ambao ulikuwa ni msimu wake wa kwanza kuwa ndani ya Simba alifunga pia mabao 8 hivyo anaingia kwenye orodha ya washambuliaji waliofunga mabao mengi Simba kwa muda mfupi.

Anakutana na staa mwingine ambaye  ni Clatous Chama huyu ni kiungo mshambuliaji ambaye alikuwa wa kwanza kutambulishwa Yanga rasmi Julai Mosi alitambulishwa kuwa ni njano na kijani anaungana na  kiungo mkongwe eneo la ukabaji anaitwa Jonas Mkude.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka.