>

MAMIA WAJITOKEZA KUMZIKA KIBAO VIONGOZI CHADEMA WAMLILIA – VIDEO

Mamia ya waombolezaji wamejitokeza Jijini Tanga katika safari ya mwisho ya aliyekua kada wa Chadema Ali Kibao aliyeuawa na mwili wake kukutwa eneo la Ununio Jijini Dar es Salaam wananchi.

Viongozi wa Vyama mbalimbali wamehudhuria msiba huo Ikiwemo Waziri wa Mambo ya Ndani Mhandisi Hamadi Masauni Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kaskazini Godbless Lema, Katibu Mkuu wa Chama hicho, Mwenyekiti Mstaafu wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe na wengineo.

Katika hotuba yake Freeman Mbowe amemtaka Waziri Masauni kumshauri Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kuunda tume ya kijaji kuchunguza matukio ya mauaji na utekaji nchini akisema kuwa kazi hiyo haitaweza kufanyika na Jeshi la Polisi pekee.

Marehemu Kibao aliyekua mjumbe wa Sekretariati ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) alifariki jana ambapo mwili wake uliokotwa katika eneo la Kawe-Ununio Jijini Dar es Salaam.

Mwili wa Marehemu Ali Kibao unatarajia kuzikwa leo katika eneo la Sahare njia ya kuelekea Wilaya ya Pangani mkoani humo.