>

NYOTA YANGA NJE MIEZI MITATU

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Bara, Yanga chini ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi watakosa huduma ya kiungo wao wa kazi Farid Mussa.

Ikumbukwe kwamba Yanga ilitwaa taji hilo la ligi msimu wa 2023/24 na ilimaliza ligi ikiwa namba moja na pointi 80 kibindoni baada ya kucheza mechi 30 za ligi.

Ni Farid Mussa atalazimika kuwa nje ya uwanja kwa takribani miezi miwili hadi mitatu kutokana na kufanyiwa upasuaji wa misuli iliyochanika nyuma ya goti.

Makamu wa Rais wa klabu hiyo Arafat Haji, amemtembelea mchezaji huyo hospitalini ili kumjulia hali nyota huyo ambaye alikuwa anavaa jezi namba 17 itakayotumika na nyota Clatous Chama.

Yanga imecheza mchezo mmoja wa ligi ilikuwa dhidi ya Kagera Sugar Uwanja wa Kaitaba, baada ya dakika 90 ubao ulisoma Kagera Sugar 0-2 Yanga.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Dizo Click.