>

MWAMBA ADEBAYO APEWA TUZO YA MVP

MSHAMBULIAJi mpya wa Singida Black Stars Victorien Adebayo amepewa tuzo ya ufungaji bora na mchezaji bora, (MVP) kutokana na uwezo alionao ndani ya uwanja kwenye kucheka na nyavu.

 Mshambuliaji raia wa Nigeria alikuwa anatajwa kuwa kwenye rada za Simba kwa muda mrefu mpango huo umekwama na mwisho yupo Bongo akiwa Klabu ya Singida Black Stars inayonolewa na Kocha Mkuu, Patrick Aussems wengi hupenda kumuita uchebe.

Ofisa Habari wa Singida Black Stars, Hussen Masanza ameweka wazi kuwa Adebayo hakuwa katika timu awali kwenye maandalizi ya msimu mpya wa 2024/25 kutokana na ruhusa aliyokuwa ameiomba ambayo ilikuwa inajulikana.

“Tulimtambulisha Adebayo kwenye sikukuu yetu ya Big Day mapema mwezi wa 8 na tunawafahamisha kuwa tayari mchezaji Adebayo ameshawasili nchini. Mchezaji amechelewa kidogo kutokana na dharula ambayo ilikuwa inatambuliwa, kuchelewa kwake kumeathiri kidogo program ya maandalizi ya msimu kwa kuwa hakuwepo kwenye pre season.

“Lakini hayo benchi la ufundi litajua namna gani ataweza kufikia pale ambapo wamefikia lakini ni mchezaji mzuri ambaye amekuwa kwenye ubora katika ligi ya Nigeria na tunafahamu changamoto ya kumpata mchezaji huyu kutokana na uhitaji wake sokoni lakini kutokana na umahiri wa timu yetu ya scout ilifanikisha kupatikana kwake.

“Nyota wetu huyu mpya yupo Tanzania na pengine anaweza kuwa MVP na Top Score mpya ndani ya ligi yetu 2024/25 kupitia Singida Black Stars.”