>

JKT TANZANIA YATOSHANA NGUVU NA AZAM FC

WAJEDA JKT Tanzania wametoshana nguvu na matajiri wa Dar, Azam FC kwenye mchezo wa ufunguzi kwa timu zote mbili msimu wa 2024/25.

Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Meja Isahmuyo umesoma JKT Tanzania 0-0 Azam FC hivyo wababe hawa wawili wamegawana pointi mojamoja.

Kwenye mchezo wa leo timu zote mbili kipindi cha pili ziliongeza kasi ya mashambulizi kutafuta nafasi ya kupata bao lakini milango ilikuwa migumu.

Kona ya kwanza Azam FC msimu wa 2024/25 imepigwa na Idd Suleiman maarufu kwa jina la Nado ilikuwa dakika 56 lakini haikuleta matunda kwenye mchezo huo.

James Akamiko jaribio lake la dakika ya 90 liliokolewa na kipa wa JKT Tanzania kama ilivyokuwa kwa Mustapha Mohamed kipa wa Azam FC ambaye naye aliokoa jaribio la Maka Edo akiwa nje ya 18 kwa shuti ambalo lililenga lango.

Ingizo jipya eneo la ushambuliaji ndani ya JKT Tanzania akitokea Simba alipata nafasi ya kuanza mchezo wake wa kwanza dakika ya 88 akichukua nafasi ya Ilanfya.