>

SABABU YA SAMATTA KUTOITWA STARS YATAJWA, JOB AJUMUISHWA

KIKOSI cha timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars kitaingia kambini Agosti 28 2024 ambapo kutakuwa na mechi mbili kujiandaa na michezo ya kufuzu AFCON 2025 dhidi ya Ethiopia na Guinea itaayochezwa Septemba 4 na Septemba 14 2024.

Kaimu Mkuu wa Taifa Stars, Hemed Suleiman Morocco amesema kuwa wachezaji wanaitwa kwenye timu kulingana na mahitaji ya mechi husika pamoja na uwezo wake.

“Tunawaita wachezaji kutokana na mahitaji ya timu ambapo kulingana na mchezo husika wachezaji wanaitwa. Kuhusu Mbwana Samatta bado yupo katika timu ila hata mchezo uliopita hakuitwa nimeongea naye bado yupo kulikuwa kuna masuala fulanifulani ambayo tayari yamekwisha hivyo akihitajika ataitwa.”

Orodha ya wachezaji hao hii hapa:-

Ally Salim Simba

Aboutwalib Mshery Yanga

Yona Amos Pamba Jiji

Lusajo Mwaikenda Azam FC

Nathaniel Chilambo Azam FC

Mohamed Hussein Simba

Dickson Job wa Yanga

Pascal Msindo wa Azam FC

Ibrahim Hamad Bacca wa Yanga

Bakari Nondo wa Yanga

Nickson Kibabage wa Yanga

Abdulmalick Zakaria wa Mashujaa

Adolf Mtasingwa wa Azam FC

Himid Mao wa Talaal El Geish ya Misri

Novatus Dismas wa Goztepe ya Uturuki

Mudathir Yahya wa Yanga

Hussein Semfuko wa Coastal Union

Edwin Balua wa Simba

Feisal Salum wa Azam FC

Wazir Junior wa Dodoma Jiji

Cyprian Kachwele wa Vancouver Whitecaps ya Canada

Clement Mzize wa Yanga

Abel Josiah wa TDS TFF Academy.