KIVUMBI kinatarajiwa kuendelea leo Agosti 24 kwenye anga la kimataifa ambapo kuna mechi kwa timu za Afrika Mashariki zitakuwa kazini kusaka ushindi ndani ya dakika 90.
Baada ya mchezo uliopita uliochezwa Uwanja wa Azam Complex Yanga kupata ushindi wa mabao 4-0 leo watakabiliana kwa mara nyingine dhidi ya wapinzani wao Vital’O itakuwa Uwanja wa Azam Complex.
Matajiri wa Dar, Azam FC wapo Rwanda watakuwa na kazi ya kusaka ushindi dhidi ya APR ya Rwanda kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex ubao ulisoma Azam FC 1-0 APR.
Wawakilishi wa Kombe la Shirikisho Wagosi wa Kaya Coastal Union wanakibarua chakusaka ushindi dhidi ya FC Bravos kwa kuwa mchezo wa kwanza walipoteza.
Mchezo wa marudiano unatarajiwa kuchezwa Agosti 25 saa 10:00 jioni ambapo mshindi wa jumla atapatikana baada ya dakika 90.
Gor Mahia ikumbukwe kwamba walipoteza ugenini, wanakibarua cha kusaka ushindi dhidi ya Al Merreikh itakuwa Agosti 25 2024.
Ligi Kuu Bara inaendelea Agosti 24 mechi mbili zitachezwa ikumbukwe kwamba Mashujaa walitoshana nguvu bila kufungana na Tanzania Prisons Agosti 23 mchezo uliochezwa Uwanja wa Lake Tanganyika, mwisho wa reli Kigoma.
Pamba Jiji ambayo mchezo wake wa ufunguzi Agosti 16 2024 ilitoshana nguvu na Tanzania Prisons itawakaribisha Dodoma Jiji saa 10.00 jioni.
Halafu saa 1.00 usiku itakuwa Kagera Sugar dhidi ya Singida Black Stars kwenye burudani za Ligi Kuu Bara.