KITAWAKA LEO NGAO YA JAMII KATI YA MAN CITY DHIDI YA MABINGWA WA KOMBE LA FA, MAN UNITED

Pazia la Ligi Kuu England linafunguliwa rasmi leo Agosti 10, 2024 kwa mchezo mmoja wa Ngao ya Jamii kati ya Mabingwa wa Ligi Kuu England, Man City dhidi ya Mabingwa wa kombe la FA, Man United kwenye Manchester ‘Derby’

Timu hizi zitakutana takribani miezi miwili na nusu tangu fainali ya kombe la FA ambapo Manchester United iliilaza Man City magoli 2-1 katika dimba la Wembley na kutwaa kombe hilo.

Miamba hiyo ya jiji la Manchester inakutana kwa mara ya pili katika historia ya Ngao ya hisani England, mara ya kwanza ikiwa ni mwaka 2011 ambapo Man City ilichapwa mabao 3-2.

Timu hizi zimekutana mara 193 kihistoria huku Mashetani hao Wekundu wakishinda mara nyingi zaidi (79) huku Man City ikishinda mara 61 wakati mechi 53 zikimalizika kwa sare.

Hata hivyo, rekodi za hivi karibuni zinaibeba Man City ambapo katika mechi za mechi 10 za michuano yote, Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu wameibuka kidedea mara 7 kuhu United ikishinda mara tatu tu hakuna sare.

17:00 | Man City vs Man United
?️ Wembley