Ndege chapa ATR 72-500 inayomilikiwa na kampuni ya Voepass ilianguka jioni ya jana katika mji wa Vinhedo, wakati ikitokea jimbo la kusini la Parana kuelekea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Sao Paulo.
Juhudi za kuipata na kuitambua miili zilikuwa zinaendelea hadi alfajiri ya leo.
Mamlaka ya ajali za anga ya Brazil, CENIPA, imetangaza kuanza uchunguzi wa ajali hiyo mara moja.
Kampuni ya ATR ambayo ndiyo iliyoiunda ndege hiyo, imesema wataalamu wake wanashirikiana na mamlaka za uchunguzi.
Takwimu zinaonesha kuwa ajali 108 za ndege zimetokea mwaka huu peke yake nchini Brazil.