AZIZ KI ABEBA TUZO YA MCHEZAJI BORA (MVP) NA KIUNGO BORA WA NBC

Kiungo mshambuliaji wa Yanga Sc, Stephanie Aziz Ki ameshinda tuzo ya mchezaji bora (MVP) wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania bara msimu wa 2023/24.

Aziz Ki ametwaa tuzo nne ambazo ni tuzo ya MVP, Kiungo bora wa Ligi Kuu, mfungaji bora wa Ligi Kuu na Tuzo ya Kikosi bora cha msimu.

Pia Aziz Ki ameshinda tuzo ya kiungo bora wa Ligi Kuu bara msimu wa 2023-24 akiwashinda Kipre Junior wa Azam Fc na Feisal Salum ‘Feitoto’ wa Azam Fc.