>

CHELSEA KUMSAJILI BEKI AARON ANSELMINO KUTOKA KLABU YA BOCA JUNIORS YA ARGENTINA

CHELSEA imefikia makubaliano na klabu ya Boca Juniors ya Argentina kwa ajili ya kumsajili beki Aaron Anselmino kwa ada ya dola milioni 20.

Aaron Anselmino (19) raia wa Argentina anatarajiwa kusafiri kwenda Uingereza siku ya Jumatatu kwa ajili ya kukamilisha vipimo vya afya na kusaini mkataba wa muda mrefu.

Beki huyo atasalia kwa mkopo kwenye timu hiyo ya Argentina hadi Januari huku tajiri ‘miluzi’ Todd Boehly akiendelea kujenga kikosi cha wachezaji wenye vipaji kwa ajili ya siku za usoni.