>

VITAL’O DHIDI YA YANGA KUCHEZA UWANJA WA AZAM COMPLEX

Kwa taarifa za awali ni kwamba mechi za kimataifa za hatua ya awali kati ya Vital’O ya Burundi na Yanga SC ya Tanzania, zinaweza kuchezwa hapahapa Tanzania kutokana na changamoto zisizo za kimichezo,

Hivyo Vital’O wanatazamia kucheza michezo yao ya awali kwenye viwanja walivyoviomba nje ya Burundi ambapo uwanja wa KMC na Azam Complex ni miongoni mwa viwanja hivyo.