>

SIMBA YAANZA KWA USHINDI HUKO

IKIWA ni mchezo wa kwanza wa kirafiki kwa Simba imepata ushindi mbele ya El Qanah Egypt kwa mabao 3-0 chini ya Kocha Mkuu, Fadlu Davids.

Kwenye mchezo huo ni Ahoua alitupia kambani mabao mawili dakika ya 14, 16 na Okejepha alitupia bao moja ikiwa ni mchezo wa kujipima nguvu.

Bado kazi ipo kwa Simba kuelekea msimu wa 2024/25 unaotarajiwa kuanza Agosti 16 2024 ambapo mabingwa watetezi wa ligi ni Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi.

Agosti 3 2024 Simba inatarajia kufanya tamasha lake la Simba Day ikiwa ni maalumu kwa ajili ya utambulisho wa wachezaji wapya na wale waliokuwa kwenye kikosi hicho msimu wa 2023/24.

Ni nchini Misri Simba imeweka kambi kwa ajili ya maandalizi kuelekea msimu mpya wa 2024/25 unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.