NAHODHA msaidizi wa YangaDickson Job ameweka wazi kuwa wapo tayari kwa mechi zote za kirafiki kimataifa ambazo watacheza nchini Afrika Kusini ikiwa ni mwendelezo wa maandalizi ya msimu wa 2024/25.
Ipo wazi kwamba Job ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Miguel Gamondi anaingia kwenye orodha ya mchezaji wa kwanza kufunga bao ndani ya Yanga msimu uliopita alifanya hivyo mbele ya KMC mchezo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.
Kwenye mchezo huo Yanga ilikomba pointi tatu mazima kwa ushindi wa mabao 5-0 ukiwa ni ushindi wa kwanza mkubwa kupatikana katika mzunguko wa kwanza.
Yanga imeshatia timu Afrika Kusini kwa ajili ya mashindano ya Mpumalanga Premier’s International Cup 2024 na Toyota Cup. Leo Julai 20 Yanga itacheza dhidi ya Augsburg kwenye Mpumalanga Premier’s International Cup 2024,
Job amesema: “Kinachotoa matokeo uwanjani ni maandalizi mazuri hivyo ambacho tunakifanya ni kuwa tayari tunaamini itakuwa hivyo kwenye mechi zetu ambazo tutacheza mashabiki watarajie mazuri zaidi.”
Chini ya Miguel Gamondi ambaye ni Kocha Mkuu wa Yanga kikosi hicho kina nyota wenye uwezo mkubwa ikiwa ni Aziz Ki, Clatous Chama, Pacome, Maxi kwenye eneo la viungo.