>

LIGI KUU MSIMU WA 2024/2025 ITAANZA AGOSTI 16, 2024

BODI  ya Ligi Kuu Tanzania, (TPLB)  wameweka wazi kuwa msimu wa 2024/2025 utaanza Agosti 16, 2024 kwa kila timu kupambania malengo yao ndani ya uwanja.

Ikumbukwe kwa msimu wa 2023/24 mabingwa wa ligi ni Yanga walitwaa taji hilo wakiwa na mechi tatu mkononi kabla ya kukamilisha hesabu kucheza mechi 30 ndani ya ligi.

Walimaliza wakiwa na pointi 80 ambapo mchezo wao wa kwanza ilikuwa dhidi ya KMC uliochezwa Uwanja wa Azam Complex hivyo wana kazi ya kupambania malengo yao kuanzia Agosti 16.

Kuna timu ambazo zilishuka daraja ni Mtibwa Sugar ya Morogoro na Geita Gold baada ya kugotea kwenye nafasi mbili za mwisho kwenye ligi.