AZIZ RASMI MALI YA YANGA, KIJANI NA NJANO UZI WAKE

MABORESHO ndani ya kikosi cha Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi yanaendelea ambapo wamemtambulisha mtu mwingine wa kazi ndani ya kikosi hicho.

Anaitwa Aziz Andambwile ambaye alikuwa anakipiga ndani ya kikosi cha Singida Fountain Gate msimu wa 2023/24.

Ipo wazi kwamba Julai 9 2024 Aziz ametambulishwa Yanga baada ya kufanyiwa vipimo vya afya tayari kwa changamotompya ndani ya mabingwa watetezi wa ligi.

Mbali na Aziz nyota wengine wapya ambao wapo ndani ya Yanga ni  Clatous Chama kiungo mshambuliaji aliyekuwa anakipiga ndani ya Simba msimu wa 2023/24.

Chama ni mchezaji wa kwanza kutambulishwa Yanga ilikuwa ni Julai Mosi 2024 alitambulishwa kuwa ni njano na kijani tayari amewasili Bongo kujiunga na wachezaji wengine kambini.

Pia Prince Dube muuaji anayetabasamu ni mali ya Yanga ambapo kasaini dili la miaka miwili yupo kambini kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya yeye alikuwa anacheza Azam FC msimu wa 2023/24 mpaka alipoomba kuvunja mkataba wake kisha akatambulishwa Yanga.