YANGA WAPOKEA KWA MSHTUKO KIFO CHA YUSUF MANJI, WATOA POLE KWA FAMILIA

Uongozi wa Yanga umesema umepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarita ya kifo cha aliyewahi kuwa Mdhamini na Mwenyekiti wa klabu hiyo, Yusuf Manji.

Taarifa iliyotolewa na Club hiyo imesema Kifo cha Manji kimetokea leo June 30, 2024 Nchini Marekani alipokuwa akipatiwa matibabu.

Rais wa Yanga, Eng Hersi Said amesema enzi za uhai wake, Yusuf Manji alikuwa Kiongozi mahiri aliyejituma na kujitoa kwa ajili ya kuijenga Club ya Yanga “Hili ni pigo kubwa kwetu Young Africans Sports Club na Familia ya michezo kwa ujumla, tutamkumbuka Yusuf Manji kwa mapenzi yake makubwa aliyokuwa nayo kwa Club yetu na namna alivyokuwa akijitoa kwa hali na mali katika kuiendeleza sekta ya michezo Tanzania”

“Ndugu Yusuf Manji alihudumu katika nafasi mbalimbali za kiuongozi ndani ya Club yetu kama Mdhamini na Mwenyekiti ambapo hadi umauti unamkuta alikuwa Mwanachama wa Young Africans Sports Club, Uongozi wa Young Africans Sports Club, unatoa pole kwa Familia, Ndugu, Jamaa, Marafiki na Wanamichezo wote Nchini kwa msiba mzito wa Mpendwa wetu, tunamuombea kwa Mwenyezi Mungu aipumzishe roho ya Marehemu mahala pema Peponi, Amina”