YANGA BINGWA WA KOMBE LA SAFARI CUP

Klabu ya Young Africans Sc imeibuka bingwa wa kombe la #Safari Cup baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Safari Champions katika dimba la Benjamin Mkapa.

FT: Safari Champions 1️⃣➖4️⃣ Yanga SC
⚽️ Omary Mfaume
⚽️ Shekhan
⚽️ Prosper
⚽ Hussein

Safari Champions ni kikosi ambacho kilipatikana kupitia programu maalum iliyoendeshwa na TBL ambayo ilitafuta vijana wenye vipaji kutoka mikoa mbali mbali na kufanikiwa kuunda timu yenye wachezaji 25.