UJERUMANI YATINGA ROBO FAINALI YA KOMBE LA MATAIFA ULAYA EURO 2024

Ujerumani imetinga hatua ya robo fainali ya kombe la Mataifa Ulaya EURO 2024 kufuatia ushindi wa 2-0 dhidi ya Denmark katika dimba la Signal lduna Park (Dortmund).

Jamal Musiala alifunga bao lake la tatu kwenye michuano hiyo mnamo dakika ya 68 baada ya Kai Havertz kuitanguliza Ujerumani kwa mkwaju wa penalti mnamo dakika ya 53’

Musiala ndio kinara wa magoli kwenye EURO 2024 mpaka sasa akiwa na magoli matatu sawa na Georges Mikautadze wa Georgia.

FT: Germany 🇩🇪 2-0 🇩🇰 Denmark
⚽ Havertz (P) 53’
⚽ Musiala 68’