Simba Day Itakuwa na balaa Kinomanoma Agosti 3 Uwanja wa Mkapa

KUELEKEA Simba Day inayotarajiwa kufanyika Agosti 3, 2024 uongozi wa timu hiyo umebainisha kuwa kutakuwa na balaa zito kinomanoma.

Ikumbukwe kwamba Hassan Dalali aliyekuwa mwenyekiti wa Simba anaingia kwenye rekodi ya waasisi wa Simba Day ambayo ilikuwa ikifanyika ifikapo Agosti 8.

Sababu kubwa ya Simba Day ni utambulisho wa benchi la ufundi, wachezaji wapya na wale waliokuwa ndani ya kikosi msimu wa 2023/24.

Ahmed Ally Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa Simba Day ya msimu huu sio ya kukosa kwa kuwa kutakuwa na mengi mazuri kwa mashabiki.

“Simba Day ya msimu huu itakuwa nzuri sana yenye balaa zito kwelikweli, kikubwa mashabiki wasikubali kuikosa hii itafana hivyo wanapaswa kuendelea na maandalizi.”

WAZIRI SILAA AINGILIA KATI SAKATA LA MAMA ALIYEDAI KIWANJA CHAKE KUCHULIWA MKOPO BENKI BILA KUJUA…